info@saratani.or.tz

Our email

+255 757 120 337

9:00 A.M. - 5:00 P.M.

Donate Now

UMUHIMU WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA KATIKA KUJIKINGA DHIDI YA SARATANI

UMUHIMU WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA KATIKA KUJIKINGA DHIDI YA SARATANI
MATUNDA NI NINI?
Matunda ni sehemu ya mmea ambayo mara nyingi ndiyo inakuwa imebeba mbegu za mmea husika. Hivyo kwa mmea, tunda ni sehemu ambako mbegu za mmea hutunzwa lakini kwetu binadamu na baadhi ya wanyama, tunda hutumika kama chakula.

MBOGAMBOGA NI NINI?
Mbogamboga kwa lugha rahisi unaweza sema ni sehemu ya mmea tofauti na tunda ambayo hutumiwa na wanadamu kama chakula.

Faida zitokanazo na matunda na mboga za majani Kwa binadamu.
Miongoni mwa faida tunazoweza kuzipata kwa kutumia matunda na mboga mboga katika maisha yetu ni pamoja na hizi zifuatazo;

1. Ni vyanzo vya vitamini. Vitamini ni moja ya vitu muhimu sana katika miili yetu ili kukua katika hali iliyo nzuri na afya bora. Vitamini hizi za asili (zisizo tengenezwa na binadamu) haziwezi kupatikana katika aina nyingine ya chakula kinyume na mazao yatokanayo na mimea. Mfano, vitamini A ipatikanayo katika matunda kama vile nyanya inasaidia mtu aweze kuona vizuri.

2. Husaidia kuimarisha kinga za miili yetu dhidi ya magojwa. Kwa kutumia matunda na mbogamboga, mtu hujengeka afya bora yenye kinga za mwili zilizoimarika dhidi ya magojwa na.

3. Matunda ni chanzo cha haraka cha nguvu (energy) mwilini. Kwa mtu ambaye amepungukiwa na nguvu mwilini ambako kunaweza sababishwa na kukaa muda mrefu bila kula, basi mtu kama huyo anashauriwa atumie baadhi ya matunda ambayo yatasaidia kuongeza nguvu mwilini mwake kwa haraka zaidi tofauti nan a akitumia vyakula vingine. Mfano; matunda kama ndizi.

4. Husaidia kuponya baadhi ya magonjwa. Kuna baadhi ya magojwa yanaweza kutibika kwa kutumia baadhi ya matunda kuliko kutumia madawa mengine kwa gharama kubwa. Mfano, ugonjwa wa ngozi uitwao ACNE, ugojwa huu wa ngozi unaweza tibika kwa kula matunda aina ya tufaha(apple) na inafaa zaidi mtu akila tufaha(apple) pamoja na maganda yake.

5. Matunda pia husaidia katika kupunguza uzito. Kwa wale wenye tatizo la uzito mkubwa wanashauriwa muda mwingine watumie matunda badala ya vyakula vingine ili kupunguza uzito na hii itafanya kazi vizuri wakiongezea na kufanya mazoezi ya mwili pia.

MATUNDA NA MBOGAMBOGA YANASAIDIAJE KATIKA KUJIKINGA DHIDI YA SARATANI?
Kitaalamu bado haijathibitika kuwepo kwa tunda au mboga za majani au mmea wowote ambao unaweza kuponya saratani, ila kwa kutumia mbogamboga na matunda inaweza ikamsaidia yule ambaye hajapata saratani katika kuepuka baadhi ya saratani. Lakini pia kwa yule mwenye saratani itamsaidia katika kujenga afya yake wakati anapewa matibabu ili aweze kupona kwa harataka. Zifuatazo ni baadhi ya faida za matunda na mbogamboga ambazo zitamsaidia mtu kuepuka saratani.

1. Kwenye baadhi ya matunda kuna kemikali ziitwazo anti-oxidants ambazo husaidia katika kutuepusha dhidi ya saratani. kemikali hizi zikifika mwilini husaidia kuondoa vitu viitwavyo free radicalsambazo kwa kawaida huwepo mwilini na zinauwezo wa kuharibu vinasaba na kusababisha mtu kuweza kupata saratani.

2. Pia kwenye mboga za majani na matunda kuna zile kambakamba (fibres). Hizi husaidia mfumo wa mmeng`enyo wa chakula ufanye kazi vizuri na kinyesi kiwezekutoka kirahisi hivyo hupunguza muda wa utumbo kukaa na chakula na hivyo kupunguza hatari ya saratani ya utumbo inayoweza kutokea kutokana na kemikali zilizopo kwenye chakula kugusana na utumbo kwa muda mrefu.

3. Kwa kuimarisha kinga za mwili inasaidia kutuepusha na magonjwa ikiwemo saratani. kunasaratani ambazo huweza kumpata mtu endapo kinga za mwili wake zikiwa dhaifu. Mfano ni saratani zinazoweza sababishwa na virusi vya HPV kama vile shingo ya kizazi na saratani ya uume.

4. Kwa kupunguza hatari ya uzito na unene uliopitiliza. Kwa kufanya hivi inasaidia kutuepusha na baadhi ya saratani, hasa zile zinazoweza sababishwa na matezi kufanya kazi kinyume na kawaida. Mfano ni saratani za matiti na baadhi ya saratani za koo la chakula (adenocarcinomas)

TACASO is dedicated to eliminating cancer as a major health problem, and improving the lives of those living with cancer

OUR ADDRESSES

address: Dar Es Salaam - Tanzania
email: info@tacaso.or.tz
phone: +255 757 120 337

SOCIAL MEDIA