info@saratani.or.tz

Our email

+255 757 120 337

9:00 A.M. - 5:00 P.M.

Donate Now

Cancer & AIDS

NAMNA UKIMWI UNAVYOWEZA PELEKEA KUPATA SARATANI
Saratani ni ugonjwa ambao hutokea baada ya seli za mwili zilizo haribika (zenye tatizo) kuanza kugawanyika kwa wingi kinyume na utaratibu wa kibaiolojia na kugawanyika huku kunakuwa kule kusikodhibitika.

UKIMWI ni kifupi cha neno upungufu wa kinga mwilini.
Haya ni magonjwa mawili ambayo yapo tofauti kabisa na yanasababishwa na vitu tofauti kabisa lakini kwa kupata ukimwi kunaweza pelekea mtu akapata saratani japokuwa kwa kupata saratani hakuwezi pelekea mtu kupata UKIMWI pia.

UKIMWI UNAPELEKEAJE MTU KUPATA SARATANI?.
Ni kweli kwamba saratani ni matokeo ya seli za mwili zilizo haribika (ambazo hazijakamilika) kuanza kugawanyika kwa wingi kinyume na utaratibu na kusikodhibitika, lakini hizi seli za mwili zisizo kamilika huzalishwa mara nyingi mwilini mwetu ila kinachosababisha wote tusipate saratani ni kuwepo kwa utaratibu maalum mwilini mwetu wa kurekebisha yale matatizo yaliyopo kwenye seli hizo zilizoharibika (DNA repair).

Ikitokea seli hizo zimeshindikana kurekebishika basi mwili kwa utaratibu maalumu huziua seli hizo zilizo haribika na kuziondoa mwilini ili kuweza kutukinga na madhara ya seli hizo kuwepo mwilini. Hiki kitendo cha kuziua na kuziondoa mwilini zile seli ambazo zimeharibika ndo kinaitwa KINGA YA MWILI. Hivyo kwa mtu mwenye ukimwi kinga za mwili wake zinakuwa zimeshuka na hivyo hata seli zile zinazohusika kuziua na kuziondoa seli hizo zilizoharibika zinakuwa zimepoteza hiyo nguvu na matokeo yake ni seli zilizoharibika kuanza kuzaliana kwa wingi kinyume na utaratibu.

Pia kuna baadhi ya saratani ambazo zinasababishwa na virusi. Virusi hivyo huweza kuleta madhara zaidi kwa mtu aliyepungukiwa kinga mwilini mwake. Hivyo ikitokea una upungufu wa kinga mwilini, basi virusi hivyo huweza kushambulia mwili na kupelekea saratani. Mfano wa saratani hizo ni saratani ya shingo ya kizazi na Saratani ya uume ambazo husababishwa na kirusi kiitwacho HPV (Human papilloma virus)

USHAURI
Mtu kuwa na UKIMWI haimaanishi kuwa lazima atapata saratani ila ni kwamba hatari yake ya kupata saratani inakuwa imeongezeka kidoogo tofauti na yule ambaye hana UKIMWI. Hii haimaanishi akate tamaa ila kunamfanya aongeze umakini katika kujitunza na kuhakikisha kinga zake hazishuki sana mpaka zikampelekea matatizo mengine ya kiafya. Na hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo,
1. Kuendelea kutumia dawa zile anazopewa hospitari zinazosaidia kuongeza nguvu za kinga zake pia (ARV)

2. Kuhakikisha anakula viziru yaani kupata mlo kamili malanyingi iwezekanavyo ili afya yake iimarike na hivyo hata kinga za mwili kuongezeka pia

3. Akumbuke kufuata na kutekeleza ushauri wote anaopewa hospitali wa namna ya kuwa na afya njema na imara.

TACASO is dedicated to eliminating cancer as a major health problem, and improving the lives of those living with cancer

OUR ADDRESSES

address: Dar Es Salaam - Tanzania
email: info@tacaso.or.tz
phone: +255 757 120 337

SOCIAL MEDIA